Kuhusu FCGH

kuhusu

FCGH ni mkataba wa kimataifa uliopendekezwa. Inategemea haki ya afya na imeendelezwa na wataalamu wa afya na sheria juu ya muongo mmoja iliyopita. Kulingana na hii FCGH Alliance imeundwa kama NGO na inaedeshwa na wanachama ambao wamekuja pamoja kuhusu haki ya kimataifa.

Huu NGO imeanzishwa chini ya sheria ya Uswisi ili kuendeleza wazo hili kuwa sheria kuboresha maisha ya watu bilioni duniani kote.

 

Kuhusu FCGH
Haki ya binadamu ya kiwango cha kufikia afya ya kimwili na ya akili itakuwa kanuni kuu ya FCGH. FCGH ilifikiriwa kwanza mwaka 2007 kama mkataba wa kimataifa – itakuwa kisheria katika nchi zote zinazojiunga nayo. Itashugulikia uhaba wa afya kati ya nchi na ndani ya nchi. FCGH, ambayo bado haijaanzishwa, itashughulikia mapungufu ya msingi katika kutekeleza haki ya afya, na itasaidia watu wote popote walipo kuwa na nafasi kuishi maisha marefu na ya afya.

Sehemu kuu ambazo FCGH utafikia ni:
1) kuboresha uwajibikaji kwa ahadi za afya katika viwango vya mitaa, kitaifa na kimataifa. Hii itahusisha ushiriki wa umma katika uamuzi wa kuhusiana na afya kutoka jamii hadi ngazi za kimataifa;
2) kuhakikisha kuwa hakuna ubaguzi na kushughulikia kupungua kwa muda mrefu na uhaba mkubwa wa afya na wa kimataifa;
3) kuongeza fedha za kitaifa na kimataifa za afya, na;
4) kuhakikisha kwamba sekta zote za jamii zinajitahidi kutekeleza haki ya afya, na hakuna (kama vile utawala wa kitaalamu au biashara) hudhoofisha haki hii.

Kuhusu muungano wa FCGH
Siku ya Desemba 10, 2017 – Siku ya Haki za Binadamu – mashirika na watu binafsi ambao waliunga mkono FCGH, walianzisha FCGH Alliance kama NGO chini ya sheria ya Uswisi kutetea na kuhakikisha ushiriki katika mchakato wa kuendeleza FCGH. Walifanya hivyo kwa sababu ilifikia wakati wa kujenga NGO inayojulikana kwa sheria kuimarisha idadi kubwa ya wafuasi wa FCGH, kusaidia watu ambao wamepata hali mbaya ya afya, kuungana na mashirika ya kiraia na kimataifa ya taasisi za afya, kuimarisha WHO, na pia kutokana na uwezo mkubwa wa msaada wa serikali ambao inaweza kupatikana.

Lengo la FCGH Alliance ni kuimarisha FCGH. Kanuni muhimu ya FCGH Alliance itakuwa ushirikiano mpana. Tunatafuta watu binafsi na mashirika duniani kote kujiunga na wanachama wetu na kushirikiana katika jitihada zetu kuhakikisha ushiriki wa mashirika ya jamii na mashirika ya kiraia, na watu ambao haki zao za afya huvunjwa. FCGH itakuwa mkataba unaozungumza na mahitaji yao, inakabiliana na matarajio yao, na kuokoa haki yao ya afya.

“FCGH ni sharti la kimaadili, kisheria, kisiasa na afya ya umma. Ni hatua inayofuata kuelekea haki ya afya”– Mark Heywood, Section 27

“Ninahimiza jumuiya ya kimataifa kuchunguza na kutambua thamani ya mkataba wa afya duniani” – Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa zamani

 

Kwa habari zaidi wasiliana na Lyla Latif